CLOUDSMEDIAGROUP KUSHIRIKIANA NA TIGO KWENYE FIESTA 2017



 Kaimu Meneja wa Masoko Tigo, William Mpinga(katikati) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa Tigo Fiesta 2017 'Tumekusomaa' leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Tigo Fiesta, Sebastian Maganga na mwakilishi toka Basata, Mrisho Mrisho.


Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Tigo Fiesta 2017, Sebastian Maganga (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa Tigo Fiesta 'Tumekusomaa' leo jijini Dar es salaam. Kushoto kwake ni Kaimu Meneja wa Masoko Tigo, William Mpinga na mwakilishi toka Basata, Mrisho Mrisho.



Mwakilishi toka Basata, Mrisho Mrisho akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa Tigo Fiesta 2017 'Tumekusomaa' leo jijini Dar es salaam. Wengine toka kushoto niMwenyekiti wa kamati ya maandalizi Tigo Fiesta 2017, Sebastian Maganga na Kaimu Meneja wa Masoko Tigo, William Mpin


Kampuni ya simu ya mtandao wa Tigo kwa kushirikiana na Clouds Media siku ya leo mbele ya waandishi wa habari imetangaza rasmi kufunguliwa kwa pazia la tamasha la kiburudani la Fiesta tamasha ambalo huwa kutanisha wateja pamoja na baadhi ya mastaa wakubwa ama wakati mwingine kuinua vipaji vya watanzania walio sehemu mbali mbali hapa nchini

Akizungumzia juu ya tamasha hilo kaimu meneja wa masoko wa Tigo William  Mpinga amesema kuwa kwa mwaka huu wao kama Tigo weamejipanga vilivyo katika kuhakikisha wateja wao wote hususani wa mikoa yote ambayo Fiesta itapita na kuzungukia wanapata burudani pamoja na kujihisi fahari wawapo kwenye huduma za Tigo pamoja na Clouds media group

Ambapo pia ametoa wito kwa watanzania wote kujitokeza kwa wingi hasa katika zoezi zima litakapoa anzishwa dirisha la usajili kwa wakati utakapotangazwa na Sisis kama Utouh news tutakuwa pamoja na wewe katika kukuhabarisha ni lini na wapi zoezi zima la usahili utakapoanzishwa

Naye mkuu wa Vipindi na uzalishaji  kutoka katika kampuni ya Clouds Sebastian Maganga amelizungumzia tamasha hilo na kusema kuwa lengo la Tamasha ni katika kuwapa burudani watanzania hivyo kamwe Clouds hawawezi kuwaangusha kwa hilo kwani kwakuwa wamekubali kuungana pamoja na kampuni ya Tigo katika kuwahudumia Watanzania wote hussani kiburudani hivyo wananchi wajipange vilivyo


‘Kauli mbiu ya Tigo Fiesta 2017 ni Tumekusoma, ikionesha sifa kuu ya Tigo kama mtandao unaoelewa zaidi mahitaji ya wateja wake nchini kote,’ Mpinga alisema.

‘Ushirikiano huu unamaanisha kuwa pamojana kuwa mtandao unaoongza kwa mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo sasa pia ndio mtandao unaosisimua zaidi nchini. Tutawaletea wasanii wenye hadhi ya kimataifa na waliojizolea sifa ndani na nje ya nchi katika msimu wa miezi mitatu iliyojaa ofa kabambe kutoka Tigo zitakazoendana na shamrashamra za furaha na kumbukumbu za muziki murwa.

Comments

Popular posts from this blog

Mvua yatatiza mpambano kati ya Simba SC na El Masri

Marubani Wawili Wapoteza Maisha kwa Ajali ya Ndege Zanzibar

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA CHANGAMOTO ZA MADAWATI YAKIJINSIA JUNE 13