AJIBU AING’ARISHA YANGA DHIDI YA CHIPUKIZI MCHEZO WA KIRAFIKI UWANJA WA GOMBANI PEMBA
Add caption |
Mabingwa watetezi wa
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara klabu ya Yanga imeendelea na mazoezi
katika uwanja wa Gombani Visiwani Pemba ambapo imeweka kambi kwa ajili
ya mechi ya Ngao ya Hisani dhidi ya Mahasimu wao wa Jadi Simba mchezo
utakaopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Agosti 23 ya Jumatano.
Wakiwa visiwani humo
wamecheza mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya timu ya Chipukizi na Yanga
kupata ushindi wa bao 1-0 likifungwa na mshambuliaji wao mpya Ibrahim
Ajibu kipindi cha kwanza.
Huu ni mwendelezo wa Ajibu kufunga
kwani kabla ya kwenda Pemba walipita visiwani Ugunja na kucheza na
Mlandege na Yanga walipata ushindi wa jumla ya mabao 2-0 yakifungwa na
Ibrahim Ajibu na Emmanuel Martin.
Kuendelea kufunga kwa Ajibu kuna
leta imani kwa mashabiki wa timu hiyo kuelekea kwenye mechi ya Dar es
salaam Derby yenye upinzani mkubwa barani Afrika
Comments
Post a Comment