SERIKALI HUPOTEZA SHILINGI BILIONI 4 KWA AJILI YA KUAGIZA DAWA .

Image result for ummy mwalimu

WAZIRI WA AFYAMAENDELEO YAJAMII JINSIA WAZEE NA WATOTO UMMY MWALIMU

 

Timoth Marko 

TAKRIBANI shilingi bilioni 4 hupotea kila mwaka  kutokana kuharibika kwa dawa zinazoagizwa nje yanchi kuja nchini TANZANIA hali inayochangiwa kutokuwepo kwa viwanda madhubuti ya uzalishaji dawa nchini.

Akizungumza katika mkutano wa wawekezaji wenye nia yakuanzisha viwanda vya madawa nchini uliofanyika jijini Dar es salaam waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu amesemakuwa  kutokana nakutokuwepo miundombinu mathubuti ya upokeaji dawa hali inayochangia dawa zinazoingia nchini kuisha muda wake nakusababishia hasara kubwa katika uagizaji wa dawa nchini .

''Tunapata changamoto ya uagizwaji wa dawa ikiwemo hali yakubadilika kwa thamani yadola kwa ajili ya kununua dawa ,hali hii hupelekea dawa nyingi kupoteza muda wake wamatumizi nakusababishia hasara serikali takribani shilingi bilioni nne katika kuagiza dawa nchini ''Alisema Waziri wa afya ummy mwalimu .

WAZIRI ummy alisema kuwa hali ya serikali kupoteza shilingi bilioni 14 imekuwa ikikosesha raha serikali nakuamua kuvipauwezo viwanda vya ndani katika kuzalisha dawa za binadamu nchini  ikiwemo viwanda vitakavyozalisha dawa za kufubaza virusi vya ukimwi ARV.

''Nchi yetu imekuwa ikiagiza dawa za binadamu zitokazo nje ya nchi zinazotibu magonjwa kama vile HIV ,TB ,MOYO,saratani  pamoja nadawa za magonjwa yasiyo ambukiza ''aliongeza WAZIRI Ummy mwalimu .


Comments

Popular posts from this blog

Mvua yatatiza mpambano kati ya Simba SC na El Masri

Marubani Wawili Wapoteza Maisha kwa Ajali ya Ndege Zanzibar

Huduma za serikali ya Marekani zakwama kwa mara nyengine