Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 08.03.2018


Joachim Low
Add caption
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionJoachim Low
Kocha wa Ujerumani Joachim Low, mwenye umri wa miaka 58, ndiye anayepigiwa upatu kumrithi Arsene Wenger kama meneja wa Arsenal iwapo raia huyo wa Ufaransa ataondoka katika klabuhiyo msimu wa joto. (ESPN)
Kuna hisia miongoni mwa wachezaji wa Gunners ya kutopendelewa wanaolipwa mishahara mikubwa katika kalbu hiyo ya ligi ya England. (Times)
Kipa wa Manchester United David de Gea bado anasubiri pendekezo la mkataba mpya licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 raia wa Uhispania kusalia na miezi 16 katika mkataba aliyonao sasa. (Yahoo)
Ryan Sessegnon (kati kati)Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRyan Sessegnon (kati kati)
Mchezaji wa Fulham Ryan Sessegnon anapendelea kuhamia Tottenham, lakini mchezaji huyo wa timu ya taifa ya England kwa wachezaji wa chini ya miaka 19 anawaniwa na pande tofuati katika ligi ya England. (mirror)
Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Everton Dominic Calvert-Lewin, huenda akaitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya England wakati Kombe la dunia likitarajiwa msimu huu wa joto. (Mirror)
Ajenti wa mchezaji wa kiungo cha kati wa Liverpool Emre Can, 'amezuia majadiliano yote' kuhusu mustakali wa mchezaji huyo mweny umri wa miaka 24 raia wa Ujerumani. (Express)
Manchester United wanapanga mazungumzo ya mkataba mpya na mchezaji wa kiungo cha mbele mwenye umri wa miaka 22 raia wa Ufaransa Anthony Martial. (ESPN)
Matumaini ya Liverpool kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Barcelona Ivan Rakitic yameingia dosari huku mabingwa wa La Liga wakiwa na dhamira ya kuendelea kumzuia raia huyo wa Croatia (AS, kupitia Talksport)
Newcastle ndio wanaopigiwa upatu kumsajili mchezaji wa Porto mwenye umri wa miaka 36 ambaye alikuwa kipa wa Uhispania Iker Casillas katika uhamisho wa bure msimu huu wa joto. (Newcastle Chronicle)

Comments

Popular posts from this blog

Mvua yatatiza mpambano kati ya Simba SC na El Masri

Marubani Wawili Wapoteza Maisha kwa Ajali ya Ndege Zanzibar

Huduma za serikali ya Marekani zakwama kwa mara nyengine