Donald Trump: Walimu Marekani wanapaswa kupewa bunduki kuwalinda wanafunzi


Rais Donald Trump katika mkutano na wanafunzi walimu na familia katika ikulu ya Whitehouse
Image captionRais Donald Trump katika mkutano na wanafunzi walimu na familia katika ikulu ya Whitehouse
Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwamba kuwapatia walimu silaha kunaweza kuzuia mashambulio ya risasi katika shule kama lile lililowaua watu 17 wiki iliopita mjini Florida.
''Mwalimu mwenye bunduki anaweza kukabiliana na washambuliaji mara moja'', alisema. Bwana Trump alitoa pendekezo hilo huku manusura wa shambulio hilo la tarehe 14 mwezi Februari wakimtaka kuhakikisha kwamba shambulio kama hilo halitokei tena.
Rais huyo wa Republican pia aliunga mkono wito wa kuwakagua wanakotoka wanunuzi wa bunduki. Manusura wengine wakati huohuo waliwataka wa bunge wa Florida kuweka udhibiti wa bunduki.
''Tutakuwa thabiti iwapo kutakuwa na ukaguzi mbali hali ya kiakili ya mtu anayetaka kumiliki bunduki''. Trump aliwaambia wanafunzi kutoka shule ya upili ya Marjory Stoneman Douglas wakati wa hafla hiyo iliorushwa hewani moja kwa moja katika ikulu ya Whitehouse.
''Haitakuwa maneno kama ilivyokuwa awali'', aliongezea. Rais huyo wa Marekani pia aliunga mkono pendekezo lililoungwa mkono na muungano wa wamiliki wa bunduki NRA .
Rais Trump akishikilia baadhi ya maandishi yake wakati wa mkutano huoHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionRais Trump akishikilia baadhi ya maandishi yake wakati wa mkutano huo
Aliaahidi kuangazia kuhusu wito kwa walimu kupewa bunduki. ''Iwapo una mwalimu ambaye ana bunduki'', alisema ''anaweza kusitisha shambulizi lolote kwa haraka. Iwapo mwalimu angemiliki bunduki , ijapokuwa najua ni swala ambalo lingezua utata, wangepewa mafunzi maalum na wangesaidia pakubwa''.
''Kusingekuwa na uhuru wa kuingia katika shule na kuanza kufyatua risasi, kwa sababu washambuliaji wangekuwa waoga''.
Majimbo kadhaa ya Marekani tayari yanaruhusu bunduki ndani ya vyuo na taasisi za elimu kulingana na tovuti ya kujihami katika vyuo. Jimbo la Florida hatahivyo halifanyi hivyo.
Baadhi ya waliohudhuria wakitoa mawazo yao kuhusu umiliki wa bunduki nchini Marekani
Image captionBaadhi ya waliohudhuria wakitoa mawazo yao kuhusu umiliki wa bunduki nchini Marekani

Comments

Popular posts from this blog

Mvua yatatiza mpambano kati ya Simba SC na El Masri

Marubani Wawili Wapoteza Maisha kwa Ajali ya Ndege Zanzibar

Huduma za serikali ya Marekani zakwama kwa mara nyengine