BAADA YA KUWATOA AL MERRIKH, TOWNSHIP ROLLERS SASA KUKIPIGA NA YANGA SIKU HII



Na George Mganga

Licha ya kupoteza mchezo wa jana kwa mabao 2-1 dhidi ya Al-Merrikh katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Township Rollers ilifanikiwa kusonga mbele katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Rollers imefanikiwa kusonga mbele kutokana mechi ya awali kuibuka na ushindi wa mabao 3-0, hivyo kuwa na aggregate ya mabao 4-2.

Timu hiyo kutoka Gaborone, Botswana, sasa itakutana na Young Africans ya Tanzania katika hatua inayofuata, mchezo ukichezwa nchini, 6 March 2018, siku ya Jummane, ambapo Yanga itakuwa mwenyeji.

Yanga nayo ilifanikiwa kuwaondoa St. Louis FC ya Sychelles kwa jumla ya mabao 2-0 na kufanikiwa kupiga hatua ya kusonga mbele

Comments

Popular posts from this blog

Mvua yatatiza mpambano kati ya Simba SC na El Masri

Marubani Wawili Wapoteza Maisha kwa Ajali ya Ndege Zanzibar

Huduma za serikali ya Marekani zakwama kwa mara nyengine