SUMATRA YAWATADHARISHA WANANCHI SIKU ZA SIKUU.
Katibu wa Mamlaka SUMATRA Osca kikoyo |
Timothy Marko.
MAMLAKA ya usafiri wa maji na nchi kavu nchini (sumatra )imewataka wananchi wanaotarajia kusafiri msimu huu wa siku kuu kuhakikisha wanafanya maandalizi ya safari zao mapema ilkuweza kuandokana na kulanguliwa tiketi na baadhi ya makampuniya mabasi wasio waaminifu .Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Katibu wa Mamlaka hiyo Osca kikoyo amesema kuwa mamlaka inawatadharisha abiria kutonunua tiketi za safari zao kutoka kwa wapiga debe au vishoka katika eneo lavituo vya mabasi ubungo au eneo jingine .
''kumekuwepo na malalamiko kwa baadhi ya abiria kwa watoa huduma wakiwa nania ovu huwakatalia abiria wasifanye bookings zao mapema jambo linalosababisha mlundikano kwa abiria pasipo kuwa na sababu nakutoa mwanya kwa vishoka kuweza kuwa laghai abiria hao ''Alisema Katibu mtendaji Osca kikoyo .
Kikoyo alisema kuwa endapo kutakuwa na matukio kukataliwa kwa abiria kufanyasafari zao abiria anapaswa kupiga namba yasimu 078611980au 07115064338 sambamba nahilomamlaka hiyo imewataka madereva kufuata kuwa waminifu kwa wateja wao .
Comments
Post a Comment