Mugabe 'akataa wito wa kumtaka ajiuzulu'
Mugabe 'akataa wito wa kumtaka ajiuzulu'
Rais wa miaka mingi
nchini Zimbabwe anaripotiwa kukataa kuandoka madarakana mara moja
licha ya kuongezeka wito wa kumtaka ajiuzulu.
Mugabe, 93 aliwekwa
chini ya kuzuizi cha nyumbani wakati jieshi lilichukua madaraka siku ya
Jumatano kufuatia mvutano kuhusu ni nani atamrithi.Hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kuhusu mazungumzo yaliyofanywa Muganbe na ujumbe kutoka kanda hiyo pamoja na mapema
Lakini taarifa zinasema kuwa amekataa kuondoka madarakani.
Kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai alisema mapema kuwa kwa manufaa ya watu Mugabe anastahili kujiuzulu mara moja.

Taarifa zinasema kuwa Mugabe ambaye alikuwa madarakani tangu nchi hiyo ipate uhuru mwak 1980 anakataa kuondoka kwa hiari kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kuandaliwa mwaka ujao.
Baadhi ya wadadisi wanasema kuwa Bw. Mugabe anaweza kujaribu kujihakikishia usalama na familia yake kabla ya kuondoka madarakani.
Maafisa wa Zanu PF mapema walikuwa wamesema kuwa Bw. Mugabe atasalia madarakani hadi ufanyika mkutano mkuu wa Chama mwezi Disemba wakati Bw. Mnangagwa atakiongoza chama na hatimaye kuwa rais
Comments
Post a Comment