PONDAMALI AWAAMBIA SIMBA WASUBIRI SASA BAO LA TAMBWE

Ikiwa ni siku mbili baada ya kutoa sare ya bao 1-1, Kocha wa Makipa wa Yanga, Juma Pondamali ‘Mensah’, amefunguka na kudai kuwa ligi haijaisha na watalipa kisasi tu na kuhakikisha wanawafunga Simba, lakini kocha huyo amedai kuwa Simba wana bahati kwa kuwa Amissi Tambwe na Donald Ngoma hawakuwepo.
Juzi Jumamosi Yanga iliwakosa baadhi ya mastraika viwembe wa timu hiyo akiwemo Amissi Tambwe na Donald Ngoma ambao wamekuwa na rekodi safi ya upachikaji mabao.

Katika mchezo huo, bao la Yanga lilifungwa na straika Mzambia, Obrey Chirwa ambapo mpaka sasa tayari amefikisha mabao matatu msimu huu lakini Emmanuel Martin alikosa nafasi adimu ambayo ingeweza kuipa ushindi Yanga.

Kocha huyo alisema mchezo huo ulikuwa na ushindani ingawa wao walipata nafasi nyingi na walishindwa kuzitumia vyema na kusababisha kuambulia alama moja.

“Juzi Simba wamelipata bao la Chirwa tu mzunguko ujao litakuwepo la Tambwe, Ngoma, Ajibu yaani watabaki kuhesabu maana hatutawapa nafasi tena ya kutufunga wajue kabisa.

“Tumepata pointi moja ila tumewakosa mengi lakini tunajipanga, Simba wajiandae kabisa kisaikolojia kwa sababu tukikutana tena wataishia kuhesabu mabao tutahakikisha kila mshambuliaji wetu anafunga na kupata ushindi wa nguvu,” alisema Pondamali.

30 Oct 2017

0 COMMENTS:

Post a Comment

:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

Comments

Popular posts from this blog

Mvua yatatiza mpambano kati ya Simba SC na El Masri

Marubani Wawili Wapoteza Maisha kwa Ajali ya Ndege Zanzibar

Huduma za serikali ya Marekani zakwama kwa mara nyengine