JESHI LA POLISI KUENDELEA NA UCHUNGUZI KULIPULIWA OFISI ZA MAWAKILI DAR
![]() |
Kamishina wa polisi Msaidizi wa Kanda Maalum DA(SAP) Lazaro MAMBO SASA |
Timothy Marko
JESHI la Polisi kanda Maalum jijini Dar es salaam limesema linaendelea kufanya uchunguzi wa kisayansi juu ya kuwepo kwa taarifa za kulipuliwa kwa ofisi za Mawakili wa kujitegemea jijini hapa kwakuwahusisha watalamu mbalimbali wa milipuko .
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Kamishina wa polisi Msaidizi wa Kanda Maalum(SAP) Lazaro Mambosasa amesema kuwa jeshi hilo linaendelea na utafiti wa kisayansi ilikuweza kubaini nini chanzo cha Mlipuko huo nakuwataka wananchi kutoa ushirikiano na jeshi hilo pindi watakapo hitaji taarifa .
''tumelipokea taarifa za kulipuliwa kwa ofisi za mawakili nasuala hili lipo katika upelelezi tishio hili linahusianisha uchanganuzi wakisayansi hivyo tunawataka wananchi kutoa ushirikiano ''Alisema Lazaro Mambo sasa
Mambo sasa aliwataka wananchi kutokurupuka kuhusiana na tukio hilo nakuwataka kuwa watulivu kusiana nasuala hilo nakusubiri uchunguzi utakapo kamilika .
Comments
Post a Comment