Posts

Showing posts from August, 2025

VIJANA KUPIGWA MSASA DIRA YA MAENDELEO 2050

  Timothy Marko  KATIKA Kukahakisha Vijana na Makundi Maalum wanakuwa na Uelewa wa Dira ya Maendeleo ya taifa 2050, Shirika la Umoja wa Mataifa linalojihusisha na Idadi ya Watu (UNFPA) limeaanzisha program Maalum ya kuwaelimisha kundi Hilo ,Juu ya Dira hiyo ya Masuala mbalimbali yanayo wakabili Vijana ikiwemo Ukosefu wa Ajira Nchini. "Ilikuhakikisha kundi hili Linapata Uelewa Juu ya malengo ya  Dira ya taifa 2050 ikiwemo kukuza Uelewa Sekta ya Tehama likuwahakikishia Vijana wanajikwamua kiuchumi kupitia Sekta ya Tehama" Amesema Naibu KATIBU Mtendaji wa Tume ya Mipango kitaifaDk Mursali Milanzi. Dk. Milanzi Ameongeza kuwa Katika kuhakikisha Wananchi wanakuza Uelewa wa Dira ya taifa 2050,Dira hii Utekelezaji wake utatekelezwa kwa Awamu. Alisisitiza Katika kuhakikisha Dira hiyo inatekezeka Tume hiyo imejiwekea Mipango ya muda mrefu na muda mfupi ilikuweza kuhakikisha Dira hiyo inatekezeka. "Mpango wa Utekelezaji wa Dira hii utakuwa tayari November Mwaka huu,nautekelezwaji w...

JAJI MUTUNGI AVIONYA VYAMA VYA SIASA.

Image
Timothy Marko. MSAJILI wa Vyama vya Siasa Nchini Tanzania Jaji Francis Mutungi Amewataka WenyeViti wa Vyama vya Siasa  Kuzingatia Sheria za Gharama za Uchaguzi. Akizungumza naWaandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Jaji Francis Mutungi amesema kuwa Nivyema WenyeViti wa Vyama pamoja na Wagombea wa Vyama hivyo kuweza kufanya Kampeni za kistarabu na Kujiepusha na Lugha za Matusi kipindi cha Kampeni za Uchaguzi. "Amani na Umoja wa kitaifa iwe kipaumbele kwenu,Twendeni tukawe mabalozi wa Amani" Amesema Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini Jaji Francis Mutungi. Mutungi  Ameongeza kuwa Nivyema Wenyeviti  wa Vyama vya Siasa kukuza Uelewa kwa Wagombea ilikuweza kushiki Vizuri Katika Uchaguzi Mkuu. Amesisitiza kuwa Nivyema WenyeViti wa Vyama hivyo Kujiepusha na Lugha za Matusi nakuweza kufanya Kampeni za kistarabu. Naye Mkuu wa Sehemu ya Ruzuku wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini CPA Edmund Mgasha Amewataka WenyeViti wa Vyama vya Siasa kuweka Ushaidi wa Matumizi ya Vyama vy...
Image
 

DOROTHY SEMU AJITOA MBIO ZA URAIS ACT WAZALENDO, MPINA AINGIA KWA KISHINDO

Image
  Na Timothy Marko, Dm News - MWENYEKITI wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu, ametangaza rasmi kujiondoa katika kinyang’anyiro cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa niaba ya chama hicho, akisema hatua hiyo inalenga kulinda umoja na maslahi mapana ya chama. Akizungumza mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Hakainde Hichilema, Makao Makuu ya ACT Wazalendo, Dorothy Sembu amesema kuwa amejiondoa kwenye kinyang'anyiro cha Kuwania kiti cha Urais kupitia Chama hicho kwa maslahi ya Chama cha ACT Wazalendo na Umma wa Tanzania kwaujumla. “Kwa kutambua fursa na maslahi mapana ya chama chetu, nimeamua kuondoa fomu yangu kama Mgombea Urais, na kuacha fursa hii kwa mwanachama ambaye chama kitaona anafaa kwa wakati huu.”Amesema Mwenyekiti wa Chama cha ACT -Wazalendo Dorothy Sembu. Uamuzi huo umekuja siku moja baada ya aliyekuwa Mbunge wa CCM, Luhaga Mpina, kujiunga rasmi na ACT Wazalendo. Mpina alipokewa na viongozi waandamizi wa...